Isaiah 65:8-9

8 aHili ndilo asemalo Bwana: “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana
katika kishada cha zabibu,
nao watu husema, ‘Usikiharibu,
kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’
hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;
sitawaangamiza wote.

9 bNitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,
na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,
nao watu wangu wateule watairithi,
nako huko wataishi watumishi wangu.
Copyright information for SwhKC